Kipindi cha“Misemo Anayoipenda Xi Jinping”charushwa nchini Serbia
2024-05-08 11:08:54| cri

Wakati rais Xi Jinping wa China anapofanya ziara nchini Serbia, kipindi cha “Misemo Anayoipenda Xi Jinping” toleo la kimataifa kilichotengenezwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG kinarushwa mjini Belgrade. Rais Aleksandar Vucic wa Serbia alitoa hotuba kwa njia ya video akipongeza uzinduzi wa kipindi hicho.

Kipindi cha “Misemo Anayoipenda Xi Jinping” kinaangazia mada kama vile ustawi kwa pamoja na ustaarabu wa kiikolojia, na kuchagua kwa makini vitabu vya kale vya Kichina na misemo ya kale iliyonukuliwa kwenye hotuba, makala na mazungumzo muhimu ya Rais Xi Jinping ili kuonyesha sifa za kipekee za nembo ya Kiroho za ustaarabu wa Kichina, maana ya enzi mpya na thamani ya utandawazi wa dunia.