Idadi ya waliofariki kwa mafuriko Kenya yafikia 238
2024-05-08 09:18:14| CRI

Serikali ya Kenya imesema idadi ya watu waliofariki kwa mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Kenya tangu mwezi Machi, imeongezeka hadi kufikia 238, na wengine 75 bado hawajulikani walipo.

Msemaji wa serikali Bw. Isaac Mwaura amesema watu wanane walipoteza maisha kwenye mafuriko ndani ya saa 24 zilizopita.

Bw. Mwaura amesema familia 47,000 zimepoteza makazi, na jumla ya watu laki 2.86 wameathiriwa na mvua kubwa na mafuriko nchini kote.

Amesema serikali imejipanga kulinda maisha ya waathirika na kutoa nyumba za kuishi kwa watu waliopoteza makazi.