Shughuli ya mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Serbia yafanyika Belgrade
2024-05-08 09:29:04| cri

Wakati rais Xi Jinping wa China akiwa ziarani nchini Serbia, Shirika kuu la Utangazaji la China CMG na Kituo Kikuu cha Televisheni na Redio cha Serbia RTS wameendesha shughuli ya mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Serbia mjini Belgrade. Rais Aleksandar Vucic wa Serbia ametoa hotuba kwa njia ya video akipongeza shughuli hiyo.

Naibu waziri mkuu wa Serbia Aleksandar Vulin, mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong, waziri wa utamaduni wa Serbia Nikola Selaković walitoa hotuba katika ufunguzi wa shughuli hiyo. Bw. Vulin amesema, urafiki ni matunda ya wakati, na katika miaka zaidi ya 60 iliyopita, watu wa nchi hizo mbili wameshikana mikono, na kuwa na mawasiliano ya kiutamaduni.

Bw. Shen Haixiong, amesema kwa watu wa China, Serbia ni rafiki mkubwa. Katika miaka ya hivi karibuni, CMG imefanya ushirikiano na vyombo vikuu vya habari vya Serbia. Katika kipindi kijacho, CMG pia itafanya ushirikiano zaidi na idara ya uhusiano na vyombo vya habari ya Ikulu ya Serbia, Gazeti la Politico la Serbia na kituo cha RTS cha Serbia.