Eliud Kipchoge: 'Unyanyasaji mtandaoni baada ya kifo cha Kiptum ulikuwa wakati mbaya zaidi maishani mwangu'
2024-05-08 22:32:43| cri

Bingwa mara mbili wa Olympiki wa mbio za Marathon, Eliud Kipchoge, ameeleza jinsi alivyoteseka mitandaoni kufuatia kifo cha mshika rekodi ya dunia wa mbio za marathon, Kelvin Kiptum, katika ajali ya barabarani Februari mwaka huu.

Kwenye mahojiano na BBC Sports, Kipchoge alisema kuwa alipoteza asilimia 90 ya marafiki zake baada ya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kudai kwamba kwa namna fulani alihusika na kifo cha nyota huyo wa mbio za marathon.

Kipchoge alisema kuwa katika kipindi hicho, alihofia maisha yake na ya familia yake kutokana na kile kilichovuma mitandaoni, huku akipewa vitisho vya kuchoma kambi yake huko Kaptagat, biashara yake mjini Eldoret, na nyumba yake.

Kiptum alifariki katika ajali ya barabarani mnamo Februari pamoja na kocha wake Gervais Hakizimana kando ya barabara ya Eldoret-Eldama Ravine.