Wakati Rais Xi Jinping wa China alipofanya ziara nchini Ufaransa, pande hizo mbili zimetoa Taarifa ya Pamoja Kuhusu Hali ya Mashariki ya Kati, kufikia maoni ya pamoja kuhusu masuala makuu ya kanda hiyo zikiwemo mgogoro kati ya Palestina na Israel, suala la nyuklia la Iran na mgogoro wa Bahari Nyekundu. Taarifa hiyo imeonesha maadili ya binadamu na matakwa ya jumuiya ya kimataifa ya kulinda haki na usawa, na uwajibikaji wa China na Ufaransa zikiwa nchi kubwa wa kulinda amani na utulivu wa dunia, na pia kuingiza msukumo muhimu kwa ufumbuzi wa masuala ya nyeti ya Mashariki ya Kati.
Zikiwa nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, China na Ufaransa zinaafikiana juu ya masuala mengi ya Mashariki ya Kati. Wakati wa ziara yake hiyo nchini Ufaransa, rais Xi alizungumzia mara nyingi mgogoro kati ya Palestina na Israel, akisisitiza kuwa mgogoro huo unaoendelea hadi sasa ni mtihani kwa maadili ya binadamu, na kwamba jumuiya ya kimataifa ni lazima ichukue hatua. Pia ameeleza kuwa, kipaumbele kwa sasa ni kusimamisha vita kwa pande zote, kuhakikisha uokoaji wa kibinadamu, na ufumbuzi wa mgogoro huo ni “Mpango wa Nchi Mbili”.
Kwa upande wa Ufaransa, nchi hiyo inapenda kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na China, kulinda kwa pamoja utaratibu wa pande nyingi, katiba ya Umoja wa Mataifa na sheria ya kimataifa.
Hivi sasa dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali. Wakati hali ya dunia inapozidi kuwa na misukosuko mingi, ni muhimu kwa China na Ufaransa kushikilia nia yao ya awali, na kubeba majukumu makubwa zaidi.
Taarifa ya pamoja iliyofikiwa kati ya China na Ufaransa kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, pamoja na busara na ujasiri zilizooneshwa, zinaifanya dunia itarajia kuwa, katika miaka 60 ijayo, China na Ufaransa zitashirikiana katika kuleta matumaini kwa dunia yenye matata, na kutafuta mwelekeo wa maendeleo ya binadamu.