China na Ufaransa kuendelea na ushirikiano katika miaka 60 ijayo
2024-05-08 11:11:10| cri

Rais Xi Jinping wa China aliyekuwa ziarani nchini Ufaransa tarehe 6 alizungumza na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron, na kufikia makubaliano mbalimbali ikiwemo kutoa taarifa nne za pamoja, na kusaini mikataba karibu 20 ya ushirikiano.

Katika ziara hiyo, Rais Xi amependekeza kwamba China na Ufaransa zinapaswa kushikilia nia ya awali zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi miaka 60 iliyopita, kuunda uhusiano wa kuaminiana, kuvumbua na kubeba majukumu katika zama mpya, kukinga kupingana kwa makundi, kuhimiza masikilizano ya nchi tofauti, kusukuma mbele utaratibu mpya wa dunia wenye ncha nyingi, na kupinga kutengana kwa uchumi.

Amesema hivi sasa dunia inakabiliana na mabadiliko pamoja na migogoro, na zikiwa nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, China na Ufaransa zinapaswa kubeba majukumu zaidi.

Nchi hizo mbili zimeafikiana kuzidisha mawasiliano na ushirikiano katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kulinda anuwai ya viumbe na akili bandia.

Wachambuzi wengi wanaona kuwa China na Ufaransa zinatoa uhakikisho kwa dunia kwa kudumisha utulivu wa uhusiano wao.