AstraZeneca kuondoa chanjo ya Covid-19
2024-05-09 22:54:08| cri

AstraZeneca ilisema Jumanne kwamba imeanza kuondoa chanjo yake ya COVID-19 duniani kote kwa sababu ya "ziada kubwa ya chanjo zilizorekebishwa" tangu janga hilo litokee.

Kampuni hiyo pia ilisema itaendelea kuondoa idhini ya uuzaji wa chanjo ya Vaxzevria ndani ya Ulaya kwasababu ya kupungua kwa mahitaji ya chanjo hiyo, ambayo haitengenezwi tena au kutolewa.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, awali kampuni hiyo ya Uingereza na Sweden inayotengeneza dawa hiyo, ilikiri katika nyaraka za mahakama kwamba chanjo hiyo husababisha madhara kama vile kuganda kwa damu na viwango vya chini vya chembe za damu.

Kwa mujibu wa Telegraph, ambayo ilianza kuripoti kuhusu chanjo hiyo, ombi la kampuni hiyo la kuondoa chanjo hiyo lilitolewa Machi 5 na kuanza kutumika Mei 7.