Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Serbia Aleksandar Vucic jana Mei 8 walikutana pamoja na wanahabari baada ya kufanya mazungumzo mjini Belgrade.
Rais Xi amesema China na Serbia ni marafiki wa kweli na wenzi wakubwa, nchi hizo mbili zinaaminiana kisiasa, ushirikiano halisi wenye ubora kati yao umeendelea kupanuka chini ya uratibu wa karibu, huku urafiki ukiwa umezidi kuimarika.
Rais Xi amesema baada ya kubadilishana maoni kwa kina na mwenzake Vucic, wamefikia makubaliano mengi, ambayo ni pamoja na kujenga Jumuiya ya China na Serbia yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati ili kuweka dira kwa maendeleo ya Jumuiya ya China na Serbia yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya, kushuhudia kusainiwa kwa nyaraka mbalimbali za ushirikiano, na kusukuma mbele ushirikiano kwenye sekta za uchukuzi, miundombinu ya nishati na uvumbuzi.