Shughuli ya mawasiliano ya kiutamaduni ya kuadhimisha miaka 75 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Hungary yafanyika Budapest
2024-05-09 10:19:55| cri

Wakati rais Xi Jinping wa China akifanya ziara nchini Hungary, Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG likishirikiana na Mfuko wa Uungaji Mkono na Usimamizi wa Mali wa Vyombo vya Habari wa Hungary limefanya Shughuli ya mawasiliano ya kiutamaduni ya kuadhimisha miaka 75 tangu China na Hungary kuanzisha uhusiano wa kibalozi, ikizindua miradi mbalimbali ikiwemo kupeperusha hewani filamu ya “Fursa nchini China”.

Rais wa Zamani wa Hungary Bw. Pál Schmitt amehudhuria na kuhutubia shughuli hiyo. Amesema, katika miaka 75 iliyopita tangu China na Hungary zianzishe uhusiano wa kibalozi, nchi hizi mbili siku zote zimekuwa zikiaminiana, kuungana mikono, uhusiano wa kirafiki na ushirikiano umeendelezwa siku hadi siku.

Mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong amesema, Hungary ni rafiki mkubwa wa China barani Ulaya. Katika miaka ya hivi karibuni, China na Hungary zimefanya mawasiliano mengi ya kiutamaduni, na watu wa nchi mbili hasa vijana wamezidi kuelewana na kuzidisha urafiki kati yao. CMG linajitahidi kuhimiza maelewano kati ya watu wa nchi hizi mbili, kupitia ushirikiano mpana na Mfuko wa Uungaji Mkono na Usimamizi wa Mali wa Vyombo vya Habari wa Hungary.