Urafiki imara kati ya China na Serbia wazidi kuimarishwa
2024-05-09 16:36:01| cri

Wakati rais Xi Jinping wa China alipofanya ziara nchini Serbia miaka minane iliyopita, viongozi wa nchi hizo mbili waliamua kupandisha uhusiano kati ya China na Serbia kuwa uhusiano wa kiwenzi na kimkakati katika pande zote.

Wakati rais Xi alipozuru Serbia mwaka huu, viongozi wa nchi hizo mbili wametangaza kukuza na kuzidisha uhusiano huo na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Serbia katika zama mpya. Vile vile pande hizo mbili zimesaini taarifa ya pamoja, na kuweka mipango inayohusika kwa pande zote. Serbia imekuwa nchi ya kwanza ya Ulaya inayojenga kwa pamoja na China Jumuiya ya Mustakabali wa Pamoja, hali ambayo imeonesha kidhahiri kuwa uhusiano kati ya China na Serbia una umuhimu wa kimkakati, na umaalumu na kiwango cha juu.

Ili kuelewa vizuri Jumuiya yenye Mustakabali wa Pamoja kati ya China na Serbia katika zama mpya, lazima tufahamu kuhusu njia ya nchi hizo mbili ya kuwasiliana katika muda mrefu uliopita. Baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililotokea mkoani Sichuan nchini China, Serbia ilikuwa nchi ya kwanza kutoa kiasi kikubwa cha misaada ya uokoaji, wakati wa janga la COVID-19, rais Aleksandar Vucicwa wa Serbia alipopokea timu ya wataalamu wa matibabu kutoka China, alibusu kwa upendo mkubwa bendera ya taifa la China. Kiwanda cha Chuma cha Pua cha Smederevo cha Kundi la HBIS ambacho kinaendeshwa kwa msaada wa China kimeleta faida kubwa kwa wafanyakazi wa huko, na reli kati ya Belgrade na Novi Sad iliyojengwa na kampuni ya China ambayo imefanya kazi kwa miaka miwili, imewarahisishia usafiri wa wananchi wa nchi hizo mbili Hayo yote yameonesha China na Serbia ni marafiki wa dhati. 

Ili kusaidia ujenzi wa Jumuiya yenye Mustakabali wa Pamoja kati ya China na Serbia, rais Xi ametangaza hatua sita za China katika kipindi cha mwanzo, ambazo ni Makubaliano ya Biashara Huria kati ya China na Serbia yatakayoanza kutekelezwa rasmi kuanzia Julai Mosi, na China kuwafadhili wanasayansi vijana 50 wa Serbia kuja China kufanya mawasiliano ya sayansi na utafiti. Mbali na hayo, katika miaka mitatu ijayo, China itawaalika vijana 300 wa Serbia kusomea China, na kukaribisha viwanda vya usafiri wa ndege vya nchi hizo mbili kuanzisha usafiri wa moja wa moja wa ndege kati ya Belgrade na Guanghzou. Hatua hizo zinazohusisha uchumi, biashara, sayansi, teknolojia na utamaduni, zitaingiza msukumo mpya kwa ushirikiano na mawasiliano kati ya pande hizo mbili.

Wachina husema marafiki wanaungana kutokana na udhati na haki, na Serbia pia ina msemo usemao: marafiki ni matunda ya muda. Baada ya kupitia mtihani wa mabadiliko makubwa ya hali ya kimataifa, urafiki imara kati ya China na Serbia umezidi kuimarishwa. Hatua hii itahimiza kwa nguvu mchakato wa kisasa wa nchi hizo mbili, na pia itasaidia kulinda haki na usawa ya kimataifa. Rais Vucicwa amesema, mustakabali wa Serbia utahusiana kwa ukaribu na China. Inaweza kukadiria kuwa, urafiki imara kati ya nchi hizo mbili utaonesha uhai mpya katika zama mpya.