Viongozi wa China na Zambia wabadilishana uzoefu kuhusu usimamizi wa kiuchumi
2024-05-09 08:45:46| CRI

Maofisa wa China na Zambia wamebadilishana uzoefu kuhusu usimamizi wa uchumi, na kukubaliana kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya pande mbili  katika mambo ya uchumi na maeneo mengine.

Maofisa hao wamebadilishana uzoefu huo kwenye semina iliyofanyika Jumanne kwa njia ya video kuhusu usimamizi wa uchumi, iliyohudhuriwa na wajumbe wa kamati ya kitaifa ya maendeleo na mageuzi ya China na maofisa 30 wa serikali ya Zambia.

Balozi wa China nchini Zambia Du Xiaohui amesema, China na Zambia zikiwa nchi za kusini, zina uwezekano mkubwa wa kushirikiana katika usimamizi wa uchumi.   

Amesema China  ingependa kuisaidia Zambia na maendeleo yake kufikia mageuzi ya kiuchumi,  hii ni sehemu ya juhudi za China za kusaidia nchi zinazoendelea kulinda maslahi ya pamoja. .