Rais Xi Jinping wa China na rais Tamas Sulyok wa Hungary wamefanya mazungumzo katika Ikulu ya rais huko Budapest.
Katika mazungumzo hayo, Rais Sulyok amesema, Hungary inatarajia kukuza mawasiliano na China, kuimarisha uunganishaji wa mikakati ya maendeleo, na kuhimiza miradi muhimu ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili. Pia amesema anaamini kuwa ziara hiyo ya kihistoria ya Rais Xi itahimiza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya Hungary na China kupanda katika kiwango cha juu zaidi.
Kwa upande wake, Rais Xi amesema huu ni mwaka wa 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Hungary. China inapenda kushirikiana na Hungary, kuenzi urafiki wa kijadi, kukuza kuaminiana kisiasa, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana, na kuongoza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kupanda katika ngazi ya juu zaidi.