Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Mpito la Sudan asema mapigano hayatasitishwa hadi kikosi cha RSF kitakaposhindwa
2024-05-09 09:12:01| CRI

Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Mpito la Sudan Bw. Abdel Fattah Al-Burhan, ambaye pia ni mkuu wa jeshi la Sudan(SAF) amesema hakutakuwa na mazungumzo au usitishwaji vita hadi Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kitakaposhindwa, na ndipo amani itapatikana nchini humo. Al-Burhan ametoa kauli hiyo siku moja baada ya mapigano makali kati ya pande hizo mbili kutokea katika jimbo la Kordofan Kaskazini.

Hadi sasa, mapendekezo mengi ya amani yametolewa na mashirika mbalimbali ya kimataifa yakiwemo Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kukomesha mapigano nchini Sudan, lakini yote yanaonekana kutofaulu.