Rais Xi awasili Budapest kwa ziara ya kiserikali nchini Hungary
2024-05-09 08:45:11| CRI

Rais Xi Jinping wa China amewasili nchini Hungary kwa ajili ya ziara ya kiserikali nchini humo.

Katika  hotuba ya maandishi aliyoitoa baada ya kuwasili, Rais Xi amesema China na Hungary ni marafiki na washirika wazuri wa kuaminiana, na anafurahi kufanya ziara ya kiserikali nchini Hungary kwa mwaliko wa Rais Tamas Sulyoka na Waziri Mkuu Viktor Orban.

Amesema Hungary inajulikana kwa historia yake iliyoanzia enzi na dahari na utamaduni wake unaong’aa wa hali mbalibmali, na amewasifi watu wa Hungary   wenye bidii na uwerevu.

Rais Xi pia amesema katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Hungary na watu wake wamekuwa wakipiga hatua kubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, ambayo China inayapongeza kwa dhati.