UNHCR: Wakimbizi milioni 1.3 wa Sudan Kusini warejea nyumbani katika miaka 6 iliyopita
2024-05-09 09:10:55| CRI

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema takriban wakimbizi milioni 1.33 wa Sudan Kusini wamerejea nyumbani kwa hiari tangu kusainiwa kwa makubaliano ya amani tangu mwezi Oktoba mwaka 2018 hadi mwezi Machi mwaka 2024.

UNHCR hivi karibuni imesema huko Juba kuwa watu 45,429 wa Sudan Kusini wamethibitishwa kurudi nyumbani mwezi Machi, ambayo idadi hiyo iliongezeka kwa asilimia 12 kuliko mwezi Februari.

Shirika hilo limesema sababu ya ongezeko hilo ni ukosefu wa usalama katika nchi zinazowapokea, hasa Sudan, uhaba wa chakula, ikiwa ni pamoja na kupunguzwa kwa mgao wa chakula, na ukosefu wa ajira na fursa za kujikimu. Wengi wa waliorejea mwezi Machi walitoka Sudan na Ethiopia.