Kipindi cha televisheni cha“Nukuu anazopenda Xi Jinping” chapeperushwa nchini Hungary
2024-05-09 10:18:07| cri

Wakati Rais Xi Jinping wa China akifanya ziara nchini Hungary, Hafla ya uzinduzi wa kipindi cha televisheni cha “Nukuu anazopenda Xi Jinping” iliyotengenezwa na Shirika kuu la utangazaji la China CMG imefanyika huko Budapest. Rais wa zamani wa Hungary Bw. Pál Schmitt na waziri mkuu wa zamani Bw. Péter Medgyessy wametoa pongezi kwa kipindi hicho. Kuanzia Mei 8 kipindi hicho kinapeperushwa hewani na vyombo vikuu vya habari ikiwemo kituo cha televisheni cha Hungary.

Mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong ametoa hotuba katika hafla hiyo akisema, vyombo vya habari vinatoa mchango wa kipekee katika mchakato wa kuhimiza mawasiliano kati ya nchi na watu. Kupeperushwa kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha “Nukuu anazopenda Xi Jinping” nchini Hungary kumechagua nukuu zilizotumiwa na Rais Xi Jinping wa China katika hotuba, makala na mazungumzo, zikifungua dirisha kwa marafiki wa Hungary kuelewa fikra za utawala za Xi na kuelewa vizuri zaidi busara za kichina na moyo wa kichina.