Wake wa marais wa China na Serbia watembelea jumba la makumbusho la taifa la Serbia
2024-05-09 10:18:48| cri

Bibi Peng Liyuan, mke wa rais Xi Jinping wa China akiambatana na mke wa rais wa Serbia Bibi Tamara Vucic wametembelea jumba la makumbusho la taifa la Serbia.

Wake hao wawili wa marais wametembelea kwa pamoja maonesho ya michoro bora, huku Bibi Peng akisema jumba hilo lina historia ndefu na mikusanyiko tele, na michoro iliyopo kwenye jumba hilo imeonesha ustadi maridadi na hisia nyingi.

Bibi Peng ameongeza kuwa Jumba la Makumbusho sio tu ni dirisha la kuhifadhi na kuonesha vitu vya kale, bali pia ni ukumbi wa kutangaza ustaarabu. Amesema anatarajia pande mbili za China na Serbia zitaimarisha ushirikiano na mawasiliano katika sekta ya utamaduni, na kujenga kwa pamoja daraja la mazungumzo kati ya staarabu.

Wake hao wa marais pia wametazama maonesho ya ufumaji wa mikono wa jadi wa wanawake wa Serbia, na kuzungumza na mafundi hao.