Kenya yafanya maonyesho ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika
2024-05-10 09:14:09| CRI

Kutokana na kuendelea kupanuka kwa biashara na uwekezaji kati ya China na Afrika, maonesho ya uchumi na biashara ya China na Afrika (CAETE) barani Afrika (Kenya) ya mwaka 2024 yalianza jana huko Nairobi.

Maonesho hayo yalivutia wajumbe wa ngazi ya juu kutoka mkoa wa Hunan.

Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya, Bibi Rebecca Miano alisema maonesho hayo ni ushuhuda hai wa ushirikiano na urafiki wa muda mrefu kati ya China na Afrika. Lengo halisi la maonesho hayo ni kutumika kama kichocheo cha kufungua uwezo wa Afrika ambao haujagunduliwa kwa kuunganishwa vizuri na jumuiya ya uwekezaji na biashara ya China.

CAETE ni hatua ya mwendelezo wa "mipango minane mikuu" ya mkutano wa mwaka 2018 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wa Beijing. Naibu mkuu wa mkoa wa Hunan wa China Bw. Cao Zhiqiang amesema CAETE ni nguzo muhimu ya kukuza ushirikiano kati ya China na Afrika, ambayo tayari imeleta manufaa kwa pande hizo mbili.