Maofisa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana Alhamisi walisema kwamba idadi ya vifo kutokana na shambulizi la mabomu dhidi ya kambi za wakimbizi wa ndani (IDP) huko kusini mwa nchi hiyo imeongezeka hadi 35.
Ofisi ya Uratibu wa Mambo ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema Jumanne wiki hii kwamba makombora yasiyopungua matano yameanguka katika kambi nne za wakimbizi wa ndani na maeneo ya karibu katika vitongoji vya Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.
Ili kujibu tukio hilo, mkutano wa dharura umeitishwa na gavana wa jeshi wa jimbo hilo na kuamua kufanya mipango ya mazishi kwa wahanga hao Jumamosi wiki hii.
OCHA pia imeonya hatari ya kutokea kwa milipuko mingine katika maeneo hayo wakati ambapo moja ya makombora hayo bado halijalipuka, pamoja na kuongezeka kwa uhasama katika maeneo karibu na kambi hizo.