Ijue Saratani ya Mfuko wa Mayai
2024-05-11 09:00:03| CRI

Tarehe 8 May kila mwaka ni Siku ya Saratani ya Mfuko wa Mayai, na ilianza kuadhimishwa mwaka 2003. Mara nyingi tumekuwa tukizungumzia saratani ya shingo ya kizazi ama saratani ya matiti, lakini ni mara chache sana kusikia saratani ya mfuko wa mayai, ambayo pia ni hatari sana. Saratani hii inawapata wanawake tu, na jambo la kusikitisha ni kwamba, mtu anayeugua hii saratani hawezi kuwa na dalili zozote za wazi wakati wa mwanzo, na ni mpaka pale inapokuwa imeenea ndipo dalili zinaweza kuonekana.

Jambo lingine ambalo wengi hatulifahamu ni kwamba, mwanamke anayeugua saratani ya matiti, ni rahisi sana kupata saratani ya mfuko wa uzazi, na ndio maana mwigizaji maarufu wa filamu wa nchini Marekani, Angelina Jolie, alipogunduliwa kuwa na viashiria vya saratani ya matiti, alichukua uamuzi wa kukatwa matiti yake yote mawili na pia kuondoa mirija ya uzazi na ovari. Tukio la Jolie, wakati huo, kwa sababu ni mtu maarufu, lilizusha mjadala mwingi kote duniani, lakini kwake, aliona ni hatua nzuri ya kujikinga na saratani hiyo. Katika kipindi chetu cha leo, tutakuwa na wataalamu watakaozungumzia kwa undani saratani hii ya mfuko wa mayai.