Mtoto awe na moyo dhati wa kumshukuru mama yake
2024-05-12 17:20:07| CRI

Rais Xi Jinping wa China aliwahi kukariri shairi moja lililoandikwa na mshairi wa Enzi ya Tang wa China Bw. Meng Jiao, ambalo lilisimulia hadithi kwamba mama mmoja alishona nguo kwa makini kwa ajili ya mtoto atakayefunga safari ndefu akiwa na wasiwasi juu ya mtoto wake kuwezekana kuchelewa kurudi nyumbani, na likasifu upendo wa mama kwa watoto wao na kusisitiza watoto wawe na moyo wa kuwashukuru mama zao. Rais Xi alisema kuwa shairi hiyo limeeleza hisia ya dhati ya Wachina kwa familia zao.

Rais Xi Jinping anatilia maanani hisia hiyo siku zote. Wakati wa mwaka mpya wa jadi wa China wa mwaka 2017, Rais Xi aliwahi kuwakumbusha Wachina wasisahau hisia ya dhati kwa familia zao japo kama wakiwa mbali na familia au wakiwa na kazi nyingi. Alisema kwamba ni pale tu kila familia inapokuwa nzuri, ndipo nchi na taifa vitakuwa na ustawi.