Maonyesho ya biashara kati ya China na Afrika nchini Kenya yafungwa
2024-05-13 09:17:17| CRI

Maonesho ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika (CAETE) barani Afrika ya mwaka 2024 yamemalizika mjini Nairobi, nchini Kenya, ambapo washiriki walitoa wito tena wa kuongeza uhusiano wa kibiashara kati ya China na Afrika.

Meneja mkuu wa Kuhamasisha Uwekezaji na Maendeleo ya Biashara katika Mamlaka ya Uwekezaji ya Kenya Pius Rotich amesema kuwa maonyesho hayo yalitoa jukwaa kwa makampuni ya China kuanzisha uhusiano na wenzao kutoka barani Afrika. Anatumai kuwa uhusiano ulioanzishwa katika maonyesho hayo utakuza biashara kati ya China na Afrika.

Mkurugenzi mkuu wa Afripeak Expo Kenya ambaye alikuwa miongoni mwa waandaaji wa maonyesho hayo Gao Wei amesema kuwa maonyesho hayo yalitoa maslahi makubwa kwa jamii ya wafanyabiashara wa Afrika ambao walikuwa na nia ya kuanzisha uhusiano na makampuni ya China.