China yazindua mradi wa kujitolea nchini Ethiopia kusaidia jamii za huko
2024-05-13 23:11:47| cri

Kampuni za China nchini Ethiopia zimezindua mradi wa kujitolea ili kutoa huduma bora za kujitolea katika jamii za nchini humo.

Mradi huo unaoitwa Mradi wa Kujitolea wa Kampuni za China unaoongozwa na Mfuko wa China kwa Maendeleo ya Vijijini (CFRD) ulizinduliwa rasmi ijumaa iliyopita katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Akizungumza katika halfa hiyo, makamu mkurugenzi wa Mradi huo, Yan Kun amesema, mradi huo ni sehemu ya ahadi ya kampuni za China kutimiza wajibu wake wa kijamii nchini Ethiopia na pia kuboresha urafiki kati ya watu wa China na Ethiopia.

Kampuni za China zimewekeza katika zaidi ya miradi 2,200 nchini Ethiopia, na kutoa nafasi 560,000 za ajira kwa watu wa huko.