Serikali ya Rwanda imepinga tuhuma za Burundi kuhusu kuhusika kwake na mashambulio ya makombora yaliyotokea katika stendi ya basi iliyoko katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, ijumaa iliyopita, ambapo watu 40 walijeruhiwa.
Baada ya tukio hilo, Polisi nchini Burundi na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo waliituhumu serikali ya Rwanda kwa kuhusika na mashambulio hayo, wakidai imeshirikiana na kundi la waasi la Red Tabara ambalo Burundi inadai linaungwa mkono na serikali ya Rwanda.
Katika taarifa iliyotolewa jumapili, Ofisi ya Msemaji wa Serikali ya Rwanda imepinga vikali madai hayo, na kuitaka Burundi kutatua matatizo yake ya ndani yenyewe bila ya kuihusisha Rwanda.