Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) nchini Botswana limeonyesha wasiwasi kwamba matumizi makubwa ya dawa za kuua wadudu mashambani ili kudhibiti wadudu, magugu, na magonjwa zinaweza kuongeza hatari ya kudhuru viumbe muhimu kwa afya ya mfumo wa ikolojia.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Afya ya Mimea ya Kimataifa huko Gaborone, nchini Botswana, Mwakilishi Msaidizi wa FAO Lesedi Modo-Mmopelwa amesema kila mwaka karibu asilimia 40 ya mazao ya chakula yanapotea kutokana na wadudu, magugu, na magonjwa. Amebainisha kuwa hii sio tu inaathiri uchumi, bali pia inaathiri usalama wa chakula na lishe nchini humo, hasa kwa makundi yaliyo hatarini katika jamii za vijijini ambao kwa kiasi kikubwa wanategemea kilimo.
Amesisitiza kuwa, matumizi ya dawa za kuwaua wadudu yanaweza kuhatarisha uchavushaji, madui wa asili wa wadudu, na viumbe muhimu katika mfumo wa afya wa ikolojia.