Waziri wa Afya ya nchini Afrika Kusini Joe Phaahla ameutaka umma nchini humo kuchukua tahadhari kutokana na nchi hiyo kuripoti kesi ya kwanza ya ugonjwa wa homa ya nyani ama Mpox.
Amesema kesi hiyo inahusisha mwanaume wa miaka 35 anayeishi katika mkoa wa Gauteng ambaye majibu ya vipimo vyake yaliyotolewa tarehe 9 mwezi huu yameonyesha kuwa anaugua ugonjwa huo, na mgonjwa huyo hana historia ya kusafiri nje ya nchi.
Mara ya mwisho kwa Afrika Kusini kurekodi kesi ya Mpox ilikuwa ni mwaka 2022 wakati kesi za ugonjwa huo zilienea kote duniani.