Ethiopia yapongeza uwekezaji wa China katika sekta ya nguo
2024-05-15 10:16:24| cri

Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Maendeleo ya Bustani za Viwanda nchini Ethiopia Aklilu Tadesse amesema, uwekezaji wa China ni injini muhimu katika sekta ya nguo na vitambaa nchini Ethiopia, na kwamba wawekezaji wa China ni msingi muhimu wa maendeleo ya sekta hiyo nchini Ethiopia.

Akizungumza jana wakati wa majadiliano kati ya maofisa kutoka Shirikisho hilo na Tume ya Uwekezaji ya Ethiopia pamoja na kampuni za China zinazotaka kuwekeza katika sekta ya nguo na vitambaa nchini Ethiopia.

Akizungumzia mchango mkubwa wa sekta hiyo katika uchumi wa Ethiopia, Tadesse amesema uwekezaji katika sekta hiyo ni kichocheo kikubwa cha maendeleo ya Ethiopia na ukuaji wa jumla wa uchumi, na kuongeza kuwa, sekta hiyo imetoa nafasi za kudumu na za muda mfupi za ajira kwa maelfu ya Waethiopia.