SADC yazindua kanzi data ya dawa SMD
2024-05-15 10:16:54| cri

Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) imezindua kanzi data ya dawa (SMD) ili kusaidia kila nchi mwanachama wa Jumuiya hiyo kupata taarifa ya bei ya bidhaa za afya wakati wa kufanya manunuzi.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mawaziri wa Afya wa SADC kuridhia taarifa ya mshauri mwelekezi juu ya maeneo yanayopewa kipaumbele katika utekelezaji wa mpango wa ununuzi wa pamoja wa bidhaa za afya iliyotolewa Novemba mwaka jana nchini Angola.

Kanzi data hiyo iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam, Tanzania, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya nchi hiyo, Dk John Jingu, ina umuhimu mkubwa kwa nchi wanachama wa SADC, na itawasaidia kubadilishana taarifa muhimu zinazohusu ununuzi wa bidhaa za afya kwa pamoja.