Putin kufanya ziara ya kiserikali nchini China
2024-05-15 09:30:38| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying Jumanne alitangaza kwamba kutokana na mwaliko wa Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Russia Vladimir Putin atafanya ziara ya kiserikali nchini China kuanzia Mei 16 hadi 17.

Akiongea na wanahabari msemaji mwingine wa wizara ya mambo ya nje, Wang Wenbin, amesema hii ni ziara ya kwanza ya Putin baada ya kuapishwa kuwa rais wa Russia kwa muhula mpya.

Wakati mwaka huu China na Russia zikiadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, katika ziara hiyo, Xi na Putin watabadilishana mawazo kuhusu uhusiano wa pande mbili, ushirikiano katika nyanja mbalimbali, na masuala ya kimataifa na ya kikanda wanayofuatilia kwa pamoja.

Ameongeza kuwa China itatoa taarifa muhimu kuhusu ziara hii kwa wakati ufaao.