Watu 39 wafariki kutokana na surua nchini Sudan Kusini katika miezi minne iliyopita
2024-05-15 23:15:03| cri

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema watu 39 wamefariki kutokana na ugonjwa wa surua tangu mwezi Januari nchini Sudan Kusini.

Katika ripoti yake ya magonjwa ya mlipuko iliyotolewa jijini Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, Shirika hilo limesema kesi 2,271 zinazoshukiwa kuwa na surua zimeripotiwa, huku maabara zikithibitisha kesi 146.

WHO imesema tofauti kubwa kati ya kesi zinazoshukiwa na zilizothibitishwa inaonyesha haja kubwa ya kuboresha ukusanyaji wa sampuli na upimaji katika maabara ili kuhakikisha utambuzi sahihi.

Ripoti hiyo imesema, kuboresha maeneo hayo kutasaidia uchunguzi wa kiufanisi wa mlipuko na taarifa, na kuruhusu miongozo ya ufanisi ya afya ya umma na ukusanyaji wa rasilimali.