Misri yafanya jaribio la kwanza la teksi zinazotumia umeme katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala nchini humo
2024-05-16 10:57:44| cri

Misri imefanya jaribio la kwanza la matumizi ya teksi zinazotumia umeme katika Mji Mpya wa Utawala wa nchi hiyo, kwa lengo la kutoa chaguo la uafiri wa kisasa na rafiki wa mazingira.

Awamu hiyo ya kwanza imehusisha teksi 10 zinazotumia umeme zilizopelekwa katika Mji huo mpya, ambao kwa sasa ni makazi ya wizara nyingi na taasisi za serikali ya Misri.

Teksi hizo zinazomilikiwa na Wizara ya Uchukuzi ya Misri, zitajumuisha magari 85 yaliyotengenezwa na kampuni ya MG4 ya China na magari 60 ya kampuni ya Chevrolet Bolt, na zitasimamiwa na kampuni ya ndani ya Misri.

Licha ya usalama, pendekezo hilo linaendana na msukumo wa Misri wa kuwa na suluhisho la kisasa na endelevu la uchukuzi.