Marais wa China na Russia wasaini Taarifa ya Pamoja kuhusu kuimarisha uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote katika zama mpya
2024-05-16 15:24:21| cri

Rais Xi Jinping wa China leo amefanya mazungumzo na rais Vladimir Putin wa Russia ambaye yupo ziarani nchini China katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing. Viongozi hao wamesaini Taarifa ya Pamoja Kuhusu Kuimarisha Uhusiano wa Kiwenzi na Ushirikiano wa Kimkakati Kwa Pande Zote Katika Zama Mpya wakati inapotimia miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.