Meli kadhaa za Ufilipino zakusanyika kinyume na sheria karibu na kisiwa cha Huangyan cha China
2024-05-16 14:40:23| cri

Mei 16, meli kadhaa za Ufilipino zimekusanyika kinyume na sheria karibu na kisiwa cha Huangyan cha China, na kufanya shughuli zisizohusiana na uvuvi wa kawaida. Kikosi cha ulinzi wa pwani cha China kimeimarisha ufuatiliaji na usimamizi kwenye eneo hilo na kuchukua hatua kuzidhibiti meli hizo kwa mujibu wa sheria.