Warizi mkuu wa Slovakia yupo katika hali mahututi baada ya kupigwa risasi
2024-05-16 09:10:34| CRI

Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico yuko katika hali mahututi baada ya kupigwa risasi mjini Handlova, eneo la Trencin nchini Slovakia.

Mshukiwa aliyezuiliwa papo hapo anaripotiwa kuwa mzee wa miaka 71.

Shirika la habari la Slovakia TASR lilimnukuu makamu mwenyekiti wa bunge Lubos Blaha akisema kuwa tukio hilo lilitokea wakati wa kikao cha bunge. Bunge hilo limeahirishwa hadi itakapotangazwa tena.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha TA3, tukio hilo lilitokea katika mji wa Handlova, takriban kilomita 150 kaskazini mashariki mwa mji mkuu. Polisi wamefunga eneo hilo mbele ya Jumba la Utamaduni huko Handlova.