Putin awasili Beijing kwa ziara ya kiserikali
2024-05-16 09:12:44| CRI

Rais Vladimir Putin wa Russia amewasili Beijing leo Alhamisi asubuhi. Kufuatia mwaliko wa Rais Xi Jinping wa China, Putin atafanya ziara ya kiserikali nchini China kuanzia Alhamisi hadi Ijumaa.