Walinzi wa Pwani ya China watoa onyo kwa meli za Ufilipino zinazoingia bila kibali
2024-05-16 09:14:37| CRI

Walinzi wa Pwani ya China Jumatano walitoa onyo kwa njia ya redio kwa meli za Ufilipino zinazoingia kwenye maji yaliyo chini ya mamlaka ya China.

Katika siku hiyohiyo, akijibu swali la vyombo vya habari vya kigeni kuhusu boti za wavuvi za Ufilipino zinazotoka Ufilipino kuelekea kwenye maji ya jirani ya Huangyan Dao, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin, alisema kuwa Huangyan Dao siku zote ni eneo la China, na China ina mamlaka yasiyopingika juu ya Huangyan Dao na eneo lake la karibu la maji.

Aliongeza kuwa China ilifanya mpango wa nia njema mwaka 2016 kwa wavuvi wa Ufilipino kuvua kwa kuruhusu idadi ndogo ya boti ndogo za uvuvi katika maji ya karibu ya Huangyan Dao, huku ikiendelea kusimamia na kufuatilia shughuli husika za wavuvi wa Ufilipino kwa mujibu wa sheria.

Amesema iwapo Ufilipino itatumia vibaya nia njema ya China na kukiuka mamlaka ya eneo la China, China itatetea haki zake na kuchukua hatua za kukabiliana kwa mujibu wa sheria, ambapo majukumu na matokeo husika yatabebwa na Ufilipino pekee.