Xi afanya mkutano wa faragha na Putin huko Zhongnanhai
2024-05-17 09:38:03| CRI

Rais Xi Jinping wa China alifanya mkutano wa faragha na mwenzake wa Russia Vladimir Putin siku ya Alhamisi huko Zhongnanhai mjini Beijing, ambapo walikuwa na mazungumzo ya kina kuhusu masuala ya kimkakati wanayoyafuatilia kwa pamoja.

Xi alibainisha kuwa dunia inapitia mabadiliko ambayo hayajaonekana katika karne moja na kuingia katika kipindi kipya cha misukosuko na mageuzi, akiongeza kuwa katika kukabiliana na hali ya dunia inayoendelea kubadilika na kuyumba, China imedumisha azma yake ya kimkakati. Amesema China inapenda kushirikiana na Russia na nchi nyingine kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kuongoza usimamizi wa kimataifa kwenda kwenye mwelekeo sahihi, kulinda kwa pamoja usawa na haki ya kimataifa, na kuhimiza amani na maendeleo ya pamoja duniani.

Akibainisha kuwa maendeleo ya China hayawezi kuzuilika na kwamba hakuna nguvu inayoweza kuzuia ukuaji na maendeleo ya China, Putin alisema kuwa Russia inapenda kuboresha ushirikiano wake na China na nchi nyingine za Kusini duniani ili kuhimiza usawa na haki kimataifa, na kufanya kazi ili kuwa na dunia yenye usawa na yenye pande nyingi.

Viongozi hao wawili wa nchi pia walikuwa na mazungumzo ya kina kuhusu mzozo wa Ukraine.