Makubaliano ya Dar es Salaam kati ya China na Afrika" yaeleza matarajio ya pamoja ya nchi za kusini
2024-05-17 22:43:51| cri

Tarehe 17 Mei mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Njewa China Bw. Wang Yi, alipofanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bw. January Makamba mjini Beijing, alisema kuwa "Makubaliano ya Dar es Salaam kati ya China na Afrika" yaliyotolewa kwa pamoja na wataalamu kutoka nchi 50 ikiwemo China na nchi za Afrika, yameeleza matarajio ya pamoja ya nchi za kusini duniani na kuonesha ufahamu wa kina zaidi wa nchi hizo kuhusu maendeleo na mustakabali yao.