Kenya yarejesha huduma za intaneti baada ya waya za chini ya bahari kukatika
2024-05-17 09:40:15| CRI

Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) na kampuni kubwa ya simu za mkononi ya Safaricom, Alhamisi walithibitisha kurejea kwa huduma za intaneti siku nne baada ya kusitishwa kutokana na kukatika mara kwa mara kwa waya chini ya bahari.

Mamlaka hizo zilitangaza kuwa huduma ya mtandao imerejeshwa kwa uwezo wake kamili na ni thabiti baada ya watumiaji kupata kasi ndogo iliyosababishwa na kukatika kwa waya chini ya bahari katika kituo cha simu cha Mtunzini nchini Afrika Kusini siku ya Jumapili. Hata hivyo, Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya ilionya kuwa kuondoa tatizo hilo lililosababishwa na kukatika kwa waya kunaweza kuchukua muda.

Ukatikaji huo uliathiri nyaya nyingi zinazohudumia Kenya, zikiwemo za Mfumo wa Nyaya za Chini ya Bahari wa Afrika Mashariki (EASSy) na nyaya za Seacom.