Marais wa China na Russia wahudhuria ufunguzi wa shughuli ya “Miaka ya Utamaduni ya China na Russia”
2024-05-17 09:31:53| CRI

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Vladimir Putin wamehudhuria ufunguzi wa shughuli ya “Miaka ya Utamaduni ya China na Russia” na tafrija ya kuadhimisha miaka 75 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Russia Alhamisi hapa Beijing.

Akibainisha kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, Rais Xi amesema historia ya uhusiano huo katika miaka 75 iliyopita inaonyesha kuimarisha na kuendeleza ujirani mwema na urafiki wa kudumu, uratibu wa kimkakati wa kina, na ushirikiano wa kunufaishana unatumikia masilahi ya kimsingi ya nchi hizo mbili na watu wake, na kuendana na matarajio ya jumuiya ya kimataifa na mwelekeo wa nyakati, ambao una umuhimu usioweza kubadilishwa. Kufanya shughuli ya “mwaka wa utamaduni” katika kila nchi ni desturi nzuri kati ya watu na ni mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Russia, vilevile ni kipengele muhimu katika historia ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, ambao unakaribishwa sana na watu wa nchi hizo mbili.

Inaaminika kuwa kauli mbiu hii itaongeza msukumo mpya katika kuendeleza urafiki kati ya China na Russia kutoka kizazi hadi kizazi na kuongeza maelewano na kujenga uhusiano wa karibu kati ya watu wake.