Vyombo vya habari vya Afrika vyahimizwa kukumbatia teknolojia ya kidijitali ili kubadilisha fikra potofu kuhusu Afrika
2024-05-17 09:30:29| CRI

Mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa Umoja wa Afrika Leslie Richer amesema vyombo vya habari vya Afrika vinapaswa kutumia nguvu ya teknolojia ya kidijitali kueleza hadithi ya Afrika, na kubadilisha masimulizi na mitazamo kuhusu bara hilo duniani kote.

Akitoa wito huo kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 3 wa Vyombo vya Habari vya Afrika (AMC), uliofanyika mjini Accra, nchini Ghana, Bi. Richer alisema kwa kutumia zana za uchambuzi wa data, vyombo vya habari vya Afrika vinaweza kuthibitisha chanzo na uhalisi wa data zinazotumika kuelezea na kutathmini bara na watu wake duniani, na kusahihisha kauli zisizo sahihi. Kwa teknolojia inayoendelea na mazingira ya vyombo vya habari vya kidijitali, masimulizi kuhusu Afrika na Waafrika ni muhimu zaidi. Ni lazima kuhoji chanzo cha data ambacho kinatumika kufafanua na kuelezea watu wa Afrika duniani.