China ingependa kushirikiana na nchi za Kiarabu ili kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja katika ngazi ya juu zaidi
2024-05-17 09:33:11| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesema China ingependa kushirikiana na nchi za Kiarabu ili kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya pande hizo mbili katika ngazi ya juu zaidi.

Rais Xi amesema hayo alipotoa salamu za pongezi kwa Mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Al Khalifa, ambaye ni mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwa kufanyika kwa Mkutano wa 33 wa Umoja wa Nchi za Kiarabu nchini Bahrain.

Rais Xi amebainisha kuwa Umoja wa nchi za Kiarabu kwa muda mrefu umejitolea kuleta umoja na kujiimarisha katika dunia ya Kiarabu, na kuhimiza amani, utulivu na maendeleo katika Mashariki ya Kati. Zikikabiliwa na mabadiliko ya dunia, nyakati na historia katika miaka ya hivi karibuni, nchi za kiarabu zimezingatia uhuru, kuhimiza maendeleo na ustawi, kutetea haki na usawa, na kulinda amani na utulivu wa kikanda.

Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na nchi za Kiarabu ili kuendeleza moyo wa urafiki kati ya pande hizo mbili, na kuchangia katika ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Amesema Mwishoni mwa mwezi huu, mkutano wa 10 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu utafanyika mjini Beijing, hivyo ana imani kwamba pande hizo mbili zitauchukulia mkutano huo kama fursa ya kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ili kuwanufaisha vyema watu wao.