Hali mbaya ya hewa yaathiri msako wa rais wa Iran baada ya helikopta aliyopanda kuanguka
2024-05-20 08:55:40| CRI

Helikopta aliyopanda rais wa Iran Ebrahim Raisi na viongozi wengine waandamizi wa serikali imepata ajali katika mkoa wa Azerbaijan Mashariki jana jumapili.

Makamu wa rais wa Iran kuhusu Masuala ya Kiutawala Mohsen Mansouri ameliambia Shirika la Habari la nchi hiyo kuwa, eneo ambalo huenda helikopta hiyo imetua bado halijajulikana kwa uhakika, ila kazi ya uokoaji inaendelea taratibu kutokana na hali mbaya ya hewa.

Nchi jirani za kana hiyo zimeeleza wasiwasi wao kuhusu ajali hiyo na kusema zipo tayari kusaidia zoezi la uokoaji.