Watu saba wameuawa kwa kupigwa risasi katika jimbo la Eastern Cape nchini Afrika Kusini
2024-05-20 14:49:12| cri

Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini limeripoti kwamba jana tarehe 19, ufyatuaji wa risasi ulitokea katika mji wa Wollowvale katika jimbo la Eastern Cape nchini Afrika Kusini, na kusababisha vifo vya watu saba. Polisi wa jimbo hilo wanawasaka washukiwa wa mauaji hayo.

Msemaji wa polisi wa eneo hilo amesema abiria sita waliokuwa kwenye gari moja akiwemo mtoto mmoja walipigwa risasi na mtu mwingine alikutwa amekufa ndani ya gari lingine umbali wa kilomita moja hivi kutoka kwenye gari la kwanza.