Mauzo ya samaki wa Tanzania nje ya nchi kwa mwaka jana yaliongezeka kwa asilimia 40, minofu ya Sangara wa mto Nile ikichangia ongezeko hilo. Takwimu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi zinaonyesha ongezeko kutoka tani 29,467 hadi tani 41,271 za samaki na bidhaa za samaki zilizouzwa nje ya nchi kati ya Aprili 2023 na Aprili 2024.
Ongezeko hili lina maana ya kuongezeka na kwa thamani ya mauzo kutoka dola za kimarekani milioni 198.2 hadi dola za kimarekani milioni 206.6, huku mapato ya kodi ya serikali pia yakiongezeka kwa asilimia 15 hadi Sh14 .45 bilioni.
Minofu ya sangara wa Nile inaendelea kuwa bidhaa inayouzwa zaidi nje ya nchi, licha ya kupungua kidogo kwa ujazo (kutoka tani 9,191 hadi tani 8,917), lakini iliingiza mapato mengi zaidi ya dola za kimarekani milioni 53.