Rais na waziri wa mambo ya nje wa Iran wathibitishwa kufariki katika ajali ya helikopta
2024-05-20 15:14:10| cri

Shirika la Habari la Taifa la Iran na Televisheni ya Taifa ya Iran wametangaza kuwa, rais Ebrahim Raisi na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Hossein Amirabdollahian wamethibitishwa kufariki katika ajali ya helikopta. Makamu wa rais wa Iran Bw. Mohsen Mansouri pia ametoa taarifa kupitia mtandao wa kijamii akithibitisha kifo cha rais Raisi.

Televisheni ya taifa ya Iran imesema, baraza la mawaziri la Iran linafanya mkutano maalumu utakaotangaza mpango wa mazishi wa rais Raisi.

Baraza hilo limetoa salamu za rambirambi kuhusu vifo vya rais Raisi na waziri Amirabdollahian, likisema wanathibitishia taifa na watu kwamba wataendelea kufuata njia ya rais Raisi, na utawala wa taifa hautayumba.