Vyombo vya habari vya Sudan tarehe 19 viliripoti kuwa Waziri wa Biashara na Ugavi wa Sudan amesema katika kipindi cha robo cha kwanza cha mwaka huu, kiwango cha urari mbaya wa biashara nchini humo kimefikia dola bilioni 4.8 za kimarekani. Thamani ya jumla ya uuzaji nje wa bidhaa imefikia dola bilioni 3.8 za kimarekani, na thamani ya jumla ya uagizaji biadhaa kutoka nje imefikia dola bilioni 8.6 za kimarekani.
Habari zimesema mapambano yanayoendelea nchini Sudan yameathiri mfumo wa sekta ya viwanda nchini humo, na asilimia 85 ya viwanda vya Sudan vimeharibiwa. Hali hiyo inailazimisha serikali ya Sudan iagize kiasi kikubwa cha bidhaa za kimsingi kutoka nje ikiwa ni pamoja na sukari, chai, maziwa na unga wa ngano, ili kukidhi mahitaji ya ndani.