Jeshi la DRC lamuua kwa risasi kiongozi wa jaribio la mapinduzi
2024-05-20 08:54:34| cri

Msemaji wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokraisa ya Kongo (DRC) Brigedia Jenerali Sylvain Ekenge jana amesema, jeshi hilo limezima jaribio la mapinduzi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa.

Katika tukio hilo, watu wanne, waliuawa, na zaidi ya wanajeshi 40 waliokuwa na silaha walikamatwa, wakiwemo raia wa Marekani na mwingereza mmoja.

Brigedia Jenerali Ekenge amesema, watu zaidi ya 50 waliokuwa na silaha walifanya jaribio la uasi jana alfajiri, ambapo walipanga kushambulia makazi ya waziri mkuu mpya Bi. Judith Tuluka Suminwa na waziri wa ulinzi Bw. Jean Pierre Bemba, lakini walishambulia makazi ya naibu waziri mkuu Vital Kamerhe baada ya kushindwa kuthibitisha anuani za viongozi hao.

Bw. Ekenge amesema, hivi sasa hali katika mji mkuu sasa imerejea katika utulivu.