Umoja wa Mataifa waongeza juhudi za kukabiliana na kipindupindu nchini Somalia
2024-05-20 09:24:14| cri



Ofisi Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) jana imesema, imeongeza juhudi zake za kukabailiana na kipindupindu nchini Somalia, huku idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo nchini humo ikifikia 120 tangu mwezi Januari.

Ofisi hiyo imesema, kesi mpya 10,647 za kipindupindu ziliripotiwa katika majimbo 7 nchini Somalia, ikiwakilisha kiwango cha vifo cha asilimia 1.1, na kusisitiza kuwa “fedha za ziada zinahitajika ili kukidhi mahitaji ya haraka ya watu walioathirika."

OCHA imesema, mvua kubwa zinazonyesha nchini humo huenda zikafanya hali ya mlipuko wa kipindupindu kuwa mbaya zaidi, na kwamba kiwango cha vifo ni kikubwa zaidi ya kile kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambacho ni chini ya ama sawa na asilimia 1.