Waziri Mkuu wa Ethiopia azindua hospitali ya kijeshi iliyojengwa kwa msaada wa China
2024-05-20 08:56:23| CRI

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amezindua hospitali maalum ya rufaa ya jeshi la nchi hiyo katika mji wa Bishoftu, mkoni Oromia nchini humo.

Katika hafla hiyo, Waziri Mkuu huyo amesema hospitali hiyo itatoa huduma za ubora wa juu za afya ambazo awali hazikuweza kupatikana nchini humo.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Shewaye Haile amesema, hopitali hiyo ina wataalamu waliopata mafunzo nchi za nje na ina vifaa vya kisasa vya tiba vilivyotolewa na serikali ya China.